Share
Date
22 May 2024

Mtandao wa Madeni na Maendeleo Tanzania (TCDD) umeshauri mikopo yote inayokopwa na Serikali kwa shughuli za maendeleo ipitishwe na Bunge badala ya jukumu hilo kuachiwa kamati zinazomshauri Waziri wa Fedha..

Ofisa mtafiti wa utetezi wa sera kutoka Shirika la AFRODAD, Diana Mochoge amewataka wananchi kuanza kufuatilia bajeti ya Taifa na kuhoji ili wajue fedha zinazotengwa kwa ajili ya bajeti zinakwenda wapi